KILIMO BORA CHA NDIZI

Ndizi ni tunda muhimu Afrika ya Mashariki na katika nchi za joto kwa jumla hasa visiwa vya caribian. Mmea wake huitwa mgomba. Kibiolojia ndizi moja ni fuu inakua pamoja na fuu nyingine kwenye mshikano au shazi.

Ndizi zapatikana kwa aina nyingi na wataalamu huhesabu takriban 100. Kwa matumizi ya kibinadamu aina zifuatazo zatofautishwa kufuatana na matumizi:
◾Ndizi za kuiva zaliwa kama matunda
◾Ndizi za kupikia zapikwa kama viazi au muhogo
◾Ndizi za uzi yaani magomba hutumiwa kama uzi za kutengezea vitambaa
◾Ndizi za pori siziso na matunda wala matumizi mengine ya chakula

Makabila mengi katika Afrika Mashariki yanaitegemea kama chakula kikuu. Katika kilimo ndizi inatumiwa pia kama lishe ya mifugo na mti wa kivuli katika kilimo cha kahawa. Ndizi
UtanguliziEdit

Ndizi tunda la moja ya mimea ya jenasi ya Musa, ambayo huitwa migomba. Asili yke ni maeneo ya Kusini mwa Asia, na inawezekana kwa mara ya kwanza ilikuzwa huko Papua New Guinea. Leo, ndizi hulimwa maeneo mengi ya tropiki.

Ndizi zipo katika familia ya Musaceae. Hulimwa hasa kwaajili ya matunda yake, na mara kadhaa kwaajili ya uzalishaji wa nyuzi na kama mimea ya mapambo. Sababu tu mimea ya ndizi, migomba, huwa mirefu na migumu kiasi, huonwa kama ni miti ya kweli, wakati ukweli ni kwamba; kutokana na muundo wa sehemu zake za ndani ya shina migomba si miti ya kweli. Mimea mingi ya aina hii, kitaalamu pseudostem, huweza hata kufikia urefu wa mita 2 – 8, na majani yake hata mpaka urefu wa mita 3.5. na ikikomaa, migomba hutoa mikungu ya ndizi zenye rangi ya kijani ambazo zikiiva hubadilika na kuwa na rangi ya manjano au wakatimwingine hata rangi nyekundu. Kasha kutoa matunda, mgomba hufa na nafasi yak e hu;chukuliwa na mgomba mwingine.

Ndizi hukua kwenye mrindikano mdogo, ujulikanao kama kichana, na kila kichana huwa na ndizi kama 20 hivi huku mkungu mmoja ukuweza kuchukua vichana 3 – 20 kwa wastani. Mkungu unaweza kufkia uzito wa kilo 30 – 50. Ndizi moja kwa wastani huwa na uzito wa gramu 125, ambayo kwa makadirio huwa na maji 75% na mada kavu 25%. Kila ndizi huwa na ganda yenye sehemu laini iliwayo ndani yake. Tena sehemu hiyo ya ndani na maganda huweza kuliwa katika hali ya ubichi au kasha kuiva. Kwa taratibu nyingi za Magharibi, sehemu ya ndani ikiwa mbichi ndiyo hupendelewa kupikwa na kuliwa, huku huko Asia ndizi na maganda yake hupikwa na kuliwa. Tunda la ndizi huwa na nyuzi nyuzi ndani yake, ambazo huwa hasa katikati ya ganda na sehemu laini ya ndani. Sehemu ya laini ya ndani ka kw=awaid ahugawanyika kwa urahisi kuanzia juu mpaka chini, kwenye sehemu tatu. Ndizi ni chanzo kizuri cha vitamini B6, vitamini C na potasiamu.

[1] ndizi aina ya Cavendish ndio hulimwa kwa wingi.

Ndizi hulimwa katika zaidi ya nchi 107 duniani. katika nchi nyingi, ndizi humaanisha zile laini na tamu ambazo huliwa kama matunda baada yam lo. Lakini pia ndizi zawezwa kukatwa na kukaushwa na kuliawa kama vile chipsi. Ndizi zilizokaushwa pia zaweza kusagwa na kupata unga wa ndizi. Ingawa baadhi ya aina ya migomba ya mwituni huwa na ndizi zenye mbegu kubwa na ngumu, ndizi zinazoliwa kwa kawaida huwa hazina mbegu. Kwa kawaida ndizi zote aidha hutumiwa zikiwa zimeiva, za njano na laini au zikiwa mbichi yaani, za kijani na ngumu kiasi. Kwa wasatani ndizi zinazouzwa biashara kimataifa ni asilimia 10 – 15 tu, huku Marekani na Uingereza wakiwa wanunuzi wakuu. Maubmile. 1.png mmea wa ndizi.

Kitaalamu ndizi huwekwa kwenye jenasi ya Musa katika familia ya Musaceae, kwenye oda ya Zingibrales.

Mmea wake usio mt kamili, huwa na urefu wa mita 6 – 7.6. majani yake hukua kuzunguka mmea na hufukia urefu wa mita 2.7 kwa urefu na sentimita 60 kwa upana. Mgomba ndiyo mmea mkubwa zaidi kuliko mimea mingine ya jamii yake. Majani yake huwa makubwa sana na huchanwa kwa urahisi sana na upepo.

Ua moja la kiume huzalishwa na kila mgomba, japo aina nyingine huweza hata kuzalisha matano ya aina hiyo mfano huko Ufilipino. Maua ya kike huzalishwa juu kabisa mwa shina na baadae hukua na kuwa tunda bila hata ya kurutubishwa. Na katika aina nyingi mbegu zimekuwa dhaifu na haziwezi tena kuzalisha mmea mwingine.

VirutubishoEdit

Matumizi mengineEdit

Ndizi kavu au zilizokaangwa baada ya kuiva huweza kuliwa kama chakula cha kutafuna. Tofauti na matunda mengine, ni vigumu kuandaa sharubati ya ndizi, na mara nyingi zinapopondwa huishia kuwa ujiuji tu.

Hata hivyo, ndizi zinabakia kuwa miongoni mwa matund matamu sana.
Maua ya ndizi baada ya kuchanua
Maua ya ndizi katika maeneo mengi yamekuwa yakitumika kama mapambo huku na wakati mweingine huliwa yakiwa mabichi au baada ya kupikwa. Shina la mgomba kwa jamii za watu hasa wa huko Asia, hupikwa na kuliwa. Maji maji yanayopatikana kisha hapo hutumika pia kutibu magonjwa ya figo na moyo.

Majani ya migomba hutumika kama sahani au vyommbo vya kuwekea chakula hasa kwa jamii tamaduni za kale na wakati wa kula vyakula vya asili. Licha ya kuhifadhi tu chakula, huambukiza ladha moja nzuri kwenye chakula.

 

Contact/ Wasiliana nasi 

Phone (Simu): +255766797400                                          Email: daudilyela@yahoo.com

Maisha Daily LogoOur Services ( Huduma zetu): 

  1. Research( Utafiti),

  2. Drip Irrigation Installation (Ufungaji wa Umwagiliaji wa Matone)

  3. Project Proposal ( Mapendekezo ya Miradi),

  4. Business Plan ( Plani za Biashara),

  5. Profit Assessment ( Upimaji wa Faida)

  6. Agricultural Books (Vitabu vya kilimo)

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s